PUGU WAVUNJA MAKUNDI YA UDIWANI


HATIMAYE  makundi ya  watia nia udiwani kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM)  Kata ya Pugu wilayani Ilala, jijini Dar es Salaam yamevunjwa rasmi kwa watia nia ambao kura za maoni hazikutosha  kumuunga mkono mgombea Udiwani wa kata hiyo  Frank Mang'ati.


Mkutano  Chama wa kuvunja makundi hayo umefanyika leo ambapo ulihudhuriwa na aliyekuwa Diwani wa Kata ya Pugu, Imelda Samjela, ambaye katika uchaguzi wa ndani wa CCM  kura zake hazikutosha.


Aliyekuwa mtia nia mwingine  ambaye alihudhuria kikao hicho ni  Magere Paul  ambapo kwa pamoja walikubaliana kumuunga mkono Mang'ati  na kuhakikisha CCM inashinda katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika  Oktoba 29 mwaka huu. 


Katika hotuba yake, Mgombea Udiwani  wa Kata ya Pugu, Mang'ati, amesema ni wakati wa Wana CCM katika kata hiyo kushikamana kuhakikisha   anashinda.