Mahawanga, Amo wang'ara kura za maoni ubunge viti maalumu Dar

 


Na MWANDISHI WETU

Mjumbe wa Mkutano Mkuu Maalumu wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Mkoa wa Dar es Salaam, Janeth Mahawanga, ametetea kiti chake baada ya kuibuka mshindi kwa kupata kura 448  katika uchaguzi wa kura za maoni ubunge wa viti maalumu.


Mahawanga alifuatiwa na  Amina Said  Amo, ambaye ni Mkurugenzi wa Amo Foundation, aliyezoa kura 421.


Akitangaza matokeo hayo katika Mkutano Mkuu Maalumu wa UWT Mkoa wa Dar es Salaam, Msimamizi wa uchaguzi huo, Mkuu wa Mkoa  wa  Kusini Unguja, Zanzibar, Idrisa Kitwana Mustafa, amesema jumla ya wajumbe walikuwa ni 768.


Ameeleza, kura halali zilizopigwa ni 766 huku kura mbili  tu zikiharibika.


 Mustafa amemtangaza Janeth na Amo kuwa washindi katika uchaguzi huo huku, Jane Jery Ntate akishika nafasi ya tatu kwa kupata kura 300.


Wengine ni Dorith Kawa alipata kura  119, Maida Waziri (113), Mos Msindo (59), Zainab Janguo (42), Neema Kyusa(21) na Geogina Lukwambe (17).


Mustafa amewataka wajumbe wa mkutano huo kuendelea kuwa wamoja na kuvunja makundi baada ya uchaguzi huo.


Msimamizi Msaidizi wa uchaguzi huo, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, ameitaka UWT  kushikamana kuelekea uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka huu.

 

Katibu wa UWT  Mkoa wa Dar es salaam, Mgeni Otto, amesema wagombea tisa walishiriki uchaguzi huo.


Amesema uchaguzi umefanyika kwa uhuru na uwazi na kuwataka wagombea kuridhika  na matokeo, waendelee kukipigania Chama katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu.

Mahawanga, Amo wang'ara kura za maoni ubunge viti maalumu Dar Mahawanga, Amo wang'ara kura za maoni ubunge viti maalumu Dar Reviewed by Gude Media on 6:09:00 AM Rating: 5

No comments

Note: Only a member of this blog may post a comment.