Polisi Dar Yafuatilia Kundi Linalodaiwa Kupanga Vurugu Novemba 6, 2026


Na MWANDISHI WETU

Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, imesema inaendelea kufuatilia kwa karibu kundi la watu wanaodaiwa kuhamasishana ndani na nje ya mkoa huo kwa lengo la kuja jijini Dar es Salaam kufanya vitendo vya fujo, vurugu na hujuma mbalimbali vinavyodaiwa kupangwa kufanyika Novemba 6, 2026.

Katika taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Polisi imeonya kuwa litachukua hatua dhidi ya mtu au kundi lolote litakalobainika kujihusisha na mipango hiyo.

Polisi imesisitiza kuwa haitavumilia viashiria vyovyote vya uvunjifu wa amani, huku ikieleza kuwa itachukua hatua za haraka kwa mujibu wa sheria ili kukabiliana na vitendo vyovyote vya vurugu, fujo au hujuma.

Aidha, Jeshi la Polisi limewataka wananchi kuheshimu utaratibu uliowekwa na Mahakama katika kufuatilia mashauri mbalimbali yanayoendelea mahakamani.