Badala ya Kulalamika Mitandaoni, Pelekeni Malalamiko Tume ya Haki za Binadamu - Mkurugenzi Igunga


MKURUGENZI Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Igunga mkoani Tabora, Selwa Hamid amemshukuru na kumpongeza, Rais wa Jamhuri ya Muungano, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuona umuhimu wa kuanzisha Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora.

Selwa ametoa shukran na pongezi hizo, katika mafunzo kutoka katika tume hiyo, yaliyofanyika katika Ukumbi wa mikutano wa Halmashauri hiyo mjini Igunga.

Amesema Watumishi wakikosa sehemu maalumu ya kupeleka malalamiko yao hudaiwa kuyakuta katika mitandao ya kijamii jambo ambalo sio sahihi.

"Huko wanakopeleka hakuna tija na badala yake kunazua taharuki lakini kuwepo kwa Tume hii inayopokea malalamiko na changamoto za aina yoyote kuanzia ngazi ya familia ni jambo jema, hivyo Watumishi na Wananchi fikisheni changamoto zenu kwenye tume hii," amesema.