Mrakibu Mwandamizi wa Polisi, Profesa Ezekiel Kyogo kutoka Kamisheni ya Polisi Jamii Makao Makuu ya Polisi Dodoma, amewataka wanawake kuithamini na kuitunza nafasi waliyopewa na Mwenyezi Mungu ya kujenga maadili mema kwenye jamii.
Wito huo umetolewa Oktoba 11, 2026 alipokuwa akizungumza na kinamama, vijana na watoto katika kituo cha Al- Madrasatul Fattah Islamiyyah Bwawani, Kigamboni, Dar es salaam.
"Mwanamke ana nafasi kubwa sana katika kujenga maadili katika jamii kwani mama anakuwa mwalimu wakwanza kabisa hivyo ni jinsi gani mwanamuke amebeba utume na nguvu kubwa Mwenyezi Mungu amemuamini kwa hiyo nyinyi wakina mama na watoto wakike Mwenyezi Mungu amewapafursa na ushawishi mkubwa katika kutengeneza jamii yenye kuzingatia maadili", amesema Profesa Kyogo.
Kwa upande wa Konstebo wa Polisi Hamid Rashid kutoka Polisi Mkoa wa Temeke, amewahasa wakina mama na wanawake kuwa kama shamba zuri lenye rutuba ambalo linatoa mazao mazuri kwa jamii.
Kwa upande wake Issa Al Hinai Mwalimu wa Madrasa Al- Madrasatul Fattah Islamiyyah amelishukuru Jeshi la Polisi kwa kuwapatia mafunzo mazuri ambayo yatakwenda kuwa msingi mzuri wa malezi ya watoto katika jamii.


