Washiriki wa Miss Ilala Wafanya Usafi Hospitali ya Chanika


Na MWANDISHI WETU

WASHIRIKI wa shindano la kumtafuta  Miss Ilala 2026, wameshirki kufanya usafi katika Hospitali ya Serikali Nguvu Kazi, Chanika Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari baada kumaliza tukio la usafi Mratibu shindano la Miss Ilala, Diana Lucas, amesema, warembo hao wameshiriki kazi za mikono kwa kufanya usafi katika hospitali ya Nguvu Kazi, kuunga mkono agizo la  Rais Dk.Samia Suluhu Hassan la kufanya usafi.

"Warembo wa miss Ilala jumla yao 13  leo wamefanya usafi wa kupendezesha Halmashauri ya jiji    la Dar es Salaam, warembo hawa wanaweka kambi The Dreamer's wakifanya  mazoezi wakijiandaa kwa shindano Octoba 24 mwaka huu, katika ukumbi wa The Voice Tabata Kinyerezi ", amesema Diana. 

Kwa upande wake Mjumbe wa Kamati ya Miss Ilala, Yasinta Mtayabarwa, amesema kwa sasa warembo wa miss Ilala wanaweka kambi ya siku saba The Dream Chanika mpaka Octobea 17 mwaka huu, watafanya tarenti katika ukumbi wa The Dreamer's, kabla fainali Octoba 24 mwaka huu.

Yasinta amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi katika kambi ya mazoezi kuangalia shindano hilo katika ukumbi wa The Dreamer's.

Diwani wa Kata ya Chanika, Gaudence Kashoka, amepongeza uongozi wa shindano hilo  kwa kuandaa miss Ilala mwaka huu na kuitangaza Chanika iliyopo Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam, sehemu ya kambi ya mashindano hayo.

Gaudence Kashoka, amesema Chanika ipo safi na Salama wanaendelea na usafi pamoja na kuheshimu agizo la Serikali katika kampeni hiyo ya usafi na kwa sasa pia wamejipanga pia kukabiliana na tahadhari zilizotolewa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) kuhusu uwepo mvua za El Nino.