Miss Kinondoni 2026 Yazinduliwa Rasmi


Na MWANDISHI WETU

SHINDANO la kuwania taji la urembo la Miss Kinondoni 2026, limezinduliwa rasmi Jijini Dar es Salaam.

Wanyange 15 wanatarajiwa kuingia kambini kuanza kujinoa kuwania taji hilo ambapo fainali inatarajia kufanyika Oktoba 25, mwaka huu katika Hoteli ya Serena, Jijini Dar es Salaam.

Akizungumzia maandalizi, Mkurugenzi wa Kampuni ya SPM Entertainment, Salome Kikwembe ambaye ni Mkurugenzi wa Miss Kinondoni 2026, alisema yanakwenda vizuri na wamejipanga kutoa ushindani mkubwa ikiwemo kutwaa taji ya Miss Tanzania.

Anasisitiza, warembo wataingia kambini kuanza kujifua vilivyo ambapo siku ya fainali kutakuwa na burudani kutoka kwa wasanii mbalimbali.

"Tumeshanza maandalizi ambapo warembo wataingia kambini kujinoa kwa mashindano, fainali ya mwaka huu itakuwa ya aina yake, tunajivunia warembo wenye sifa ambao wana uwezo wa kupambana na kutwaa taji la Miss Tanzania," anasema.