Na MWANDISHI WETU
Diwani wa Kata ya Buyuni, Jesca Mohmoud, amewasilisha taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya chama cha Mapinduzi (CCM) kwa kipindi cha Januari mpaka Juni 2026.
Akizungumza katika hafla ya kutoa taarifa hiyo, Jesca amesema mambo aliyofanya ikiwemo miundombinu ya Barabara, Sekta ya afya, sekta ya Elimu, Vyeti vya kuzaliwa, Vitamburisho vya Taifa (NIDA).
"Kata ya Buyuni inakwenda kuwa kata ya kisasa kwa kutatua kero za wananchi na kupokea miradi mikubwa ya maendeleo ya Dkt. Samia Suluhu Hassan "amesema Jesca.
Jesca ametumia fursa hiyo ya kuwasilisha Ilani, kwa kuwashukuru wapiga kura na viongozi wa chama cha Mapinduzi CCM wa matawi na ngazi ya kata ambapo alisema Kata ya Buyuni inaenda kuwa kata ya kisasa kazi kubwa imefanywa na Serikali.
Amesema Serikali imejenga Kituo cha Afya Buyuni katika Zahanati fedha zilizopelekwa kwa ajili ya utekelezaji mradi wa jengo la Wazazi na jengo la upasuaji shilingi milioni 300.
Akizungumzia miundombinu ya barabara ambapo amesema miundombinu ni sekta muhimu katika mipango ya Maendeleo ya wananchi kwa kuwa sekta hiyo mtambuka ambapo amesema kwa kutambua umuhimu wake Serikali imewekeza kiasi cha sedha nyingi.
Amesema katika kuimalisha kujenga barabara mpya na kukarabati zilizopo sambamba ujenzi wa madaraja makubwa madogo na vivuko.




