Balozi Mulamula Amlilia Mama Fatma Karume - GUDE MEDIA

Breaking

GUDE MEDIA

Kila Sauti, Habari ni Yetu Sote

Subscribe Us

ads header

9/22/26

Balozi Mulamula Amlilia Mama Fatma Karume


Na MWANDISHI WETU

Mjumbe Maalumu wa Masuala ya wanawake, Amani na Usalama wa Umoja wa Afrika (AU), Balozi Liberata Mulamula, ametoa salamu za pole kufuatia kifo cha Mama Fatma Karume, aliyekuwa mjane wa Rais wa kwanza wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Hayati Sheikh Abeid Amani Karume.

Balozi Mulamula amesema, amepokea taarifa hizo kwa masikitiko makubwa ya kuondokewa na Mama Fatuma Karume, ambapo ametoa pole kwa familia, ndugu, jamaa na viongozi wa serikali.

"Ni habari ya kusikitisha sana maana nilipata bahati ya kumuona sio zamani sana. Mwenyezi Mungu ailaze roho yake mahali pema,peponi", amesema.

Taarifa hiyo ya kifo imetolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk.Samia Suluhu Hassan, kupitia taarifa yake ya salama za rambirambi.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.