RC Tanga: Wastaafu Lindeni Mafao Yenu, Tumieni Mifumo ya Kidijitali - GUDE MEDIA

Breaking

GUDE MEDIA

Kila Sauti, Habari ni Yetu Sote

Subscribe Us

ads header

9/19/26

RC Tanga: Wastaafu Lindeni Mafao Yenu, Tumieni Mifumo ya Kidijitali

Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Balozi Dkt. Batilda Burian, akizungumza katika semina ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watmishi wa Umma (PSSSF) kwa maofisa Rasilimaliwatu wa mkoani humo, Septemba 17, 2026 kuwaelimisha huduma mbalimbali zitolewazo na mfuko na kuwahamasisha kuwasilisha madai ya wanachama kwa wakati na matumizi ya kidigitali.

Na Mwandishi wetu, Tanga

Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Balozi Dkt. Batilda Burian amewataka wastaafu kulinda mafao yao dhidi ya matapeli, huku akiupongeza Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) kwa kuhamasisha matumizi ya mifumo ya kidijitali inayorudisha heshima na tabasamu kwa wastaafu.

Akifungua semina ya PSSSF kwa waajiri iliyofanyika jijini Tanga iliyowakutanisha Maafisa Rasilimaliwatu na Utawala 120 kutoka taasisi mbalimbali za Serikali, Balozi Dkt. Batilda alieleza kuwa maboresho hayo yanaendana na maagizo ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kutoa huduma bora, za haraka na bila vikwazo. "Niwapongeze sana PSSSF kwa hatua hii inaowezesha Mafao kulipwa kwa haraka," alisema.

Meneja wa PSSSF Kanda ya Kaskazini Mashariki, Bw. Kwame Temu, aliwahimiza waajiri kutoa taarifa za watumishi wapya ndani ya siku 30 ili wasajiliwe mapema na kuwahamasisha watumishi kutumia kikamilifu mifumo ya kielektroniki. Kwa upande wake, Afisa Mfawidhi wa Mkoa wa Tanga, Hanim Babika, alisisitiza waajiri kufanyia kazi changamoto ya kugongana kwa taarifa na kuhakikisha wafanyakazi wa mikataba kusajiliwa.

Akitoa ushuhuda, Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga, Bw. Rashid Mchatta alisema elimu inayotolewa na PSSSF imebadili kabisa maisha ya wastaafu wa sasa, kwani wanatoka utumishi wakiwa wanajiamini na wenye uelewa mpana wa uwekezaji. "Sekretari wangu alipostaafu, alikuja ofisini kwangu mwenye furaha, ananieleza habari za fursa za uwekezaji tu baada ya kupata mafunzo ya PSSSF," alisema Katibu Tawala.

PSSSF inaendelea kuwasihi wanachama na wastaafu nchini kutumia mifumo rasmi ya kielektroniki ili kupata huduma kwa haraka, uwazi na usalama zaidi ambayo ni PSSSF Member Portal na PSSSF Kiganjani, aidha wawawe na changamoto kutumia simu ya bure kuwasiliana na Mfuko ambazo ni 0800110055.

Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Balozi Dkt. Batilda Burian (katiakti) akiwa na Meneja wa PSSSF Kanda ya Kaskazini Mashariki, Kwame Temu na maofisa wa mfuko huo,  washiriki wa semina ya PSSSF kwa maafisa Rasilimaliwatu na Utawala wa mkoa wa Tanga.


Washiriki wa semina ya PSSSF kwa maofisa Rasilimaliwatu na Utawala wakifuatilia mada katika semina hiyo.


No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.