TPDC Yatenga Bilioni 100 Uendelezaji Utafiti wa Utoaji Taarifa za Mitetemo Kutambua Miamba chini ya Uso wa Dunia


Shirika la Maendeleo la  Petrol Nchini  (TPDC) imetenga zaidi ya Bilioni 100 za  uendelezaji wa utafiti wa utoaji wa taarifa za mitetemo ya kutambua miamba iliyopo chini ya uso wa Dunia.

Utafiti huo unafanywa kwenye mikoa ya Lindi na Mtwara ambapo umeamza tangu miaka kadhaa iliyopita, huku ukamilikaji wake unatarajia kukamilika ifikapo mwezi Desemba mwaka huu.

Hayo yalisemwa na Mjihorojia kutoka Shirika la Maendeleo la Petrol Nchini (TPDC), Samweli Magambo alipokuwa katika Maonesho ya Kimataifa ya 50 ya Biashara, maarufu Saba Saba yanayoendelea,  Barabara ya Kilwa, Dar es salaam.

Magambo amesema kwa sasa utafiti huo, umeanza kufanya kazi ya kugundua miamba iliyopo chini ya uso wa dunia na kujua jihorojia yake ya kujua ni miamba ipi ambayo inauwezo wa kuifadhi mafuta, kuzuia mafuta yasitoke, miamba inayoweza kuzalisha mafuta na upatikanaji wa gesi asilia.

Amesema shirika hilo inamiradi mingi ambapo kwa sasa ina mradi mkubwa unaojulikana Weaswembele ambao mradi huo na miradi mingine inaendeshwa kwa kutumika fedha zake za ndani.

Amesema miradi hiyo ipo katika mikoa mitano ambayo ni Shinyanga, Simiyu, Tabora, Singida na Manyara.