DC Mpogolo Awaagiza Halmashauri na TARURA Kuzibua Mitaro Kariakoo


Na MWANDISHI WETU

MKUU wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo, ameagiza Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam kwa kushirikiana na Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini ( TARURA), kuzibua chemba zote za kupitisha maji Kariakoo. 

Mpogolo, ametoa agizo hilo Dar es Salaam, Septemba 12, 2026, katika kampeni endelevu ya usafi wa kila Jumamosi uliowashirikisha kampuni za usafi, KAJENJERE, SATEK, TIRIMA  na wafanyabishara wadogo 'Wamachinga'. 

"Natoa agizo kwa Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam, kwa kushirikiana na TARURA muanze kazi ya kuzibua mifereji ya maji na kuondoa takataka zilizoziba mifereji hiyo kupelekea kushindwa kufanya kazi ya kupitisha maji ambayo italeta madhara nyakati za mvua" amesema Mpogolo 

Mpogolo amesema mamlaka za hali ya hewa wameshatangaza uwepo wa mvua kubwa za El Nino, hivyo mifereji liiyoziba italeta madhara makubwa wakati wa mvua.

Pia Mpogolo ametumia fursa hiyo kumpongeza Rais Dk.Samia Suluhu Hassan kwa wananchi wa Ilala, ambapo amesema maagizo yake aliyotoa Ilala waananchi hawawezi kumuangusha  watasimamia na kuakikisha Jiji linakuwa safi,  kwani Ilala ndio Dar es Salaam, Tanzania. 

Aidha Mpogolo amewagiza wakandarasi wa kampuni za kuzoa taka katika halmashauri hiyo, kuakikisha kila njia panda kuweka vifaa maalumu vya kubeba taka zitakapo jaa wazipeleke dampo .

Wakati huo huo aliwagiza Wafanyabishara Ilala kila mmoja kuwa na kifaa cha kuifadhia taka Dastibin kwani wao ndio wazalishaji wa taka nyingi kila siku na kupelekea kuziba mifereji ya maji .

"Tunatoa agizo kwa Wafanyabishara wote wanaofuga Takataka chini ya meza zao wakikamatwa watapewa adhabu ya kufungiwa shughuli zao za biadhara"amesema. 

Aidha pia alitoa agizo kwa barabara zote za Ilala kufunga taa barabarani  kwa ajili ya usalama na kupendezesha jiji hilo ambalo linafanya biashara masaa 24 kwa ajili ya kukuza uchumi wa nchi yetu Tanzania. 

Aliwagiza TARURA na TANROADS kuanzia sasa wasitoe Vibari ovyo vya ujenzi katika barabara badala yake watafute utaratibu mwingine.

Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania Rajabu Amiry, amesema wasanii ni sehemu ya watu kwani usafi ni kipimo cha Utu wanaendelea kuunga mkono juhudi za Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan za kulipendezesha jiji la Dar es Salaam kwa usafi na wao wasanii wa Filamu Tanzania kila Jumamosi watashiriki usafi 

Mkurugenzi wa Kampuni ya Usafi Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam KAJENJERE amepongeza Serikali pamoja na Halmashauri ambapo amesema wakishirikiana pamoja Ilala itakuwa safi  ya kisasa na kuvutia.