Waziri Katambi awasilisha taarifa ya Polisi, Magereza na Zimamoto
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Patrobas Katambi akiwasilisha Taarifa ya Jeshi la Polisi,Magereza na Zimamoto mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje Ulinzi na Usalama (NUU), inayoongozwa na Mwenyekiti wa kamati, Najma Murtaza Giga.
Kikao hicho ni Maandalizi ya Mkutano wa Pili wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, linalotarajiwa kuanza siku ya Jumanne,27 Januari,2026.
Kikao hicho kimefanyika,leo jijini Dodoma, ambapo kimehudhuriwa pia na Naibu Waziri, Ayoub Mohamed Mahmoud, Katibu Mkuu, Ally Senga Gugu, Naibu Katibu Mkuu, Dkt. Maduhu Kazi, Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, Jeremiah Katungu, Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, John Masunga, Kamishna wa Jeshi la Polisi, Liberatus Sabas, Kamishna wa Jeshi la Polisi Zanzibar, Kombo Khamis Kombo,Wakuu wa Vitengo na Idara kutoka wizarani na maofisa waandamizi kutoka vyombo vya usalama vilivyopo chini ya wizara hiyo.
Reviewed by Gude Media
on
January 16, 2026
Rating:
