Mpogolo: JMAT nendeni mkashughulikie migogoro ya kijamii kuanzia ngazi ya familia, ardhi na changamoto za mirathi
Na MWANDISHI WETU
Mkuu wa
Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo ameitaka Jumuiya ya Maridhiano na Amani
Tanzania (JMAT), kushughulikia changamoto za kijamii kuisaidia Serikali
kurudisha furaha na kuleta maridhiano katika ngazi za familia.
Mpogolo
amesema hayo Januari 14,2026 katika uzinduzi wa idara tatu mpya za jumuiya
hiyo, Karimjee jijini Dar es Salaam.
"Nendeni
mkashughulikie migogoro ya kijamii kuanzia ngazi za chini za familia,
kashughulikieni changamoto za mirathi, migogoro ya ardhi, migogoro ya ukatili
hasa ya unyanyadaji wa kijinsia maana jamii inawahitaji sana" amesema.
Mpogolo amsema
JMAT ikafanye kazi za maridhiano kwasababu ni chombo ambacho Serikali kinawategemea
kuleta maridhiano, hususan katika ngazi za familia kwakuwa wanajukumu ya malezi na kutatua changamoto, kero za kijamii.
Pia Mpogolo
ameiomba jumuiya isichoke kushirikiana na Serikali kwasababu wananchi
wanauhitaji mkubwa katika kusaidiwa kutatua changamoto zao.
Aidha
ameipongeza JMAT kwa kutoa elimu ya amani nchini, kutatua changamoto za kisiasa
na kuleta upatanisho wa dini mbalimbali pindi inapojitokeza migogoro.
Kwa upande
wa Mwenyekiti wa jumuiya hiyo, Sheikhe Alhad Mussa Salum, amesema watahakikisha
taifa linakuwa na amani muda wote kama walivyokabidhiwa kutoka kwa waasisi wa
taifa hili likiwa salama na amani.
"Hatutakubali
amani ya nchi itoweke kirahisi, tutahakikisha migogoro inapojitokeza basi sisi
kama Jumuiya tutasimama kurejesha amani hiyo" Alhad Salum.
Amesema JMAT wameona waongeze nguvu katika kuongeza idara tatu ikiwemo ya wazee, wanawake na vijana ili kuongeza nguvu katika kazi za marishiano nchini.
Reviewed by Gude Media
on
January 15, 2026
Rating:

.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)