Baraka adakwa kwa tuhuma za kumtorosha mwanafunzi wa kidato cha pili
Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, inamshikilia mkazi wa Kakongwa, Wilaya Kahama, Mkoa wa shinya, Baraka Juma, kwa tuhuma za kumtorosha mwanafunzi wa kidato cha pili.
Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na jeshi hilo, imeeleza kuwa mtuhumiwa alitenda tukio hilo, Januari 5 mwaka huu.
Kutokana na ufuatiliaji wa kina, Januari 17, 2026 mtuhumiwa huyo alikamatwa katika nyumba ya kulala wageni, Ukonga Mombasa, Dar es salaam akiwa na mwanafunzi huyo akijiandaa kuondoka naye, kwenda Kagongwa, Shinyanga.
Aidha taarifa hiyo imeeleza kuwa hatua zaidi zinachukuliwa dhidi ya mtuhumiwa kwa kushirikisha na mamlaka zingine za kisheria.
Polisi Mkoa wa Dar es salaam inatoa wito kwa wananchi kuwa halitasita kuwachukulia hatua za kisheria kwa mtuhumiwa atakaebainika kutenda makosa kama hayo.
Reviewed by Gude Media
on
January 18, 2026
Rating:
