Selwa amewataka wasimamizi wa mafundi na Kamati za ujenzi kusimama katika nafasi zao miradi ikamilike kwa wakati
Na MWANDISHI WETU, TABORA
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Igunga mkoani Tabora, Selwa Hamid amewataka Wasimamizi wa Mafundi na Kamati za ujenzi kusimama katika nafasi zao kwa lengo la kuhakikisha miradi inatekelezwa kwa wakati na kuzingatia viwango vya fedha.
Selwa ametoa wito huo, wakati wa ziara ya kukagua miradi mbalimbali katika kata za Jimbo la Manonga wilayani Igunga.
"Tujirekebishe kwenye miradi yetu na kuongeza usimamizi kwa sababu hali ya mafundi kuondoka maeneo ya ujenzi wakati unaendelea hatukubaliani nayo," amesisitiza na kuongeza kuwa:
"Ziogopeni fedha hizi za miradi kama ukoma na mambo ya udalali yasiwepo kwenye miradi, wapeni mafundi wanaofanya kazi ipasavyo", alisema.
Reviewed by Gude Media
on
January 12, 2026
Rating:




