Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa Mzinga A, akabidhi vifaa vya shule kwa wanafunzi
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mzinga A, Lucas Banga, amekabidhi ya vifaa vya shule kwa wanafunzi zaidi ya 200 wa shule za msingi na sekondari.
Akizungumza na waandishi wa habari baada vifaa hivyo, Mbaagala Mzinga, Dar es Salaam, alisema lengo la kutoa zawadi hizo ni kuhakikisha wanafunzi wenye changamaoto wasikose masomo kwa kukosa madaftari, karamu na penseli.
Banga alisema ofisi ya serikali ya mtaa kwa kutambua baadhi ya familia hazina uwezo wa kupata mahitaji ya vifaa vya shule kwa wototo wao, ndiyo maana wametumia fursa hiyo kuwapa vifaa hivyo ili wasikwame kuanza masomo yao.
"Tangu uongozi wetu uingie madarakani tumetimiza mwaka mmoja, hivyo tumeona tufurahi na wananchi wetu kwa kuwapa zawadi hii, pia hii ni moja ya utekelezaji wa Ilani ya CCM", alisema.
Alisema utaratibu wa kuwafikia walengwa ni mpango ulioratibiwa na wajumbe wa mashina kuleta idadi ya wanufaika, ingawa kulikuwa na changamoto kwa baadhi wananchi kukosa kuandikishwa na taarifa zao kukosekana.
Pia Banga alisema wameanza kwa kutoa zawadi hizo kwa wanafunzi laikini wataendelea kufanya mambo mengi mazuri kwa kuwafikia wananchi na kutoa huduma bora.
Banga alitoa rai kwa viongozi wenzake kushuka chini kwa lengo la kuwatumikia wananchi.
Kwa upande wake Mjumbe wa serikali ya mtaa huo, Omary Ngayonga, alisema wazazi wanawajibu wa kuhakikisha watoto wao wanakwenda shuleni.
"Wazazi wawasukume watoto wao waende shule na wasiishie vichakani, pia wawafuatilie kwa ukaribu kufahamu maendeleo yao", alisema.
Naye mmoja wa wazazi wa watoto hao, Mwanahawa Yasir, alipongeza Banga kwa ubunifu wake ambao umewapunguzia wananchi changamoto kubwa ya kupata vifaa shule kwa watoto wao.
Reviewed by Gude Media
on
January 10, 2026
Rating:



