MPOGOLO: Tutatekeleza agizo la Rais kuhusu maridhiano
Na MWANDISHI WETU
Mluu wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo, amesema wataendelea kutekeleza maelekezo na maagizo ya falsafa ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan ya maridhiano kulijenga Jimbo la Segerea na wilaya hiyo .
Mpogolo Amesema hayo Dar es Salaam, alipozungumza na wenyeviti wa serikali za mitaa 61 ya jimbo hilo.
Mkutano huo umeitishwa na Mbunge wa jimbo hilo, Agnesta Kaizer wa Chama cha CHAUMA kuomba ushirikiano wa kiutendaji na wenyeviti hao, ikiwa ni hatua ya kujenga maridhiano.
Mpogolo amepongeza hatua ya mbunge huyo, Agnesta na kuwa hatua hiyo ni kutekeleza maelekezo ya Rais Dk. Samia na itasaidia kujenga jimbo hilo na Wilaya ya Ilala.
“Ninyi wenyeviti mkishirikiana na mbunge na sisi shida za watu tukihangaika nazo, tukaziweka katika listi tukaona namna za kuzitatua moja baada ya nyingine tutakuwa tumegusa na watu.
"Mnambunge anaye gusa watu. Mnyororo wa uongozi unajengwa na uhusiano lakini msingi ni zile shida za watu,”amesema Mpogolo.
Kwa upande wake Agnesta, alisema lengo la mkutano huo ni kuwaomba ushirikiano wenyeviti wa serikali za mitaa na watendaji ambao wote wanatokana na Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Amesema ufanisi wa wananchi wa Jimbo la Segerea utatokana na ufanisi wa wake na watendaji hao.
“Unapokuwa ni mbunge wa jimbo utakuwa ni mbunge usiyejitambua kama hutafahamu kwamba lile kundi namba moja unalolihitaji kwa asilimia mia moja ili uweze kutuimikia wananchi kwa weledi na ufanisi ni hili kundi la serikali za mitaa,”alisema.
Ameeleza, kama mbunge asipofanya kazi na kundi hilo kwa umoja, upendo na weledi hawezi kufanikiwa, jimbo halitofanikiwa na wenyeviti hao hawatafanikiwa kwa sababu ya mahitaji, pia ushirikiano wa mbunge kufanikisha shughuli za maendeleo.
“Jambo la pili ni kuomba uashirikiano wenu, kwa sababu sasa wote tunatumikia wananchi bila kujali tofauti za kisiasa. Mitaa yote 61 inaongozwa na wenyeviti wa serikali za mitaa wa CCM lakini mimi nitawapa ushirikiano kwa asilimia miamoja,”alieleza.
Reviewed by Gude Media
on
January 06, 2026
Rating:


