Balozi Mulamula asisitiza amani na umoja 2026



Na MWANDISHI WETU

Mjumbe Maalumu wa Umoja wa Afrika kuhusu masuala ya Wanawake Amani na Usalama, Liberatha Mulamula, amewatakia Watanzania heri ya mwaka mpya huku akiwatasisitiza kuendelea kudumisha amani na umoja.

Waziri huyo Mstaafu wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mulamula ameyesema hayo alipozungumza leo, huku akiwapongeza Watanzania kwa kupokea mwaka mpya.

Amewapongeza, wananchi kwa kuvuka salama, kwa neema ya Mwenyezi Mungu, kwani sio jambo jepesi kumaliza mwaka mzima.

 "Nawatakia Watanzania wenzangu wote kheri ya Mwaka Mpya 2026. Tusherehekee kwa upendo, amani na mshikamano.

"Kama Mjumbe Maalumu wa Umoja wa Afrika kuhusu masuala ya Wanawake Amani na Usalama, wito wangu ni kwamba wanawake ni jeshi kubwa, tuna mchango mkubwa katika kudumisha amani, umoja na undugu siyo tu kwa nchi yetu Tanzania bali kwa bara letu zima la Afrika. Umoja ni nguvu," amesema.

Amewasisitiza wananchi kuendelea kuunga mkono jitihada za serikali inayoongozwa na Rais Dk.Samia Suluhu Hassan za kukuza uchumi na kufanya kazi kwa bidii kujiletea maendeleo. 
Balozi Mulamula asisitiza amani na umoja 2026 Balozi Mulamula asisitiza amani na umoja 2026 Reviewed by Gude Media on January 01, 2026 Rating: 5

Boxed Width - True/False

True