Mchengerwa aagiza uchunguzi ufanyike Hospitali ya Temeke
Waziri wa Afya, Mohamed Mchengerwa, amemuelekeza Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Dk. Seif Shekalaghe kufanya uchunguzi katika Hospitali ya Temeke, Dar es Salaam, baada kubainika utendaji usioridhisha ukiwemo kuzimwa kwa mashine ya X-ray.
Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari imeeleza kuwa hivi karibuni kumebainika utendaji usiorisha katika hospitali hiyo, ikiwa ni pamoja kuzimwa kwa mashine hiyo.
Taarifa hiyo imeeleza kuwa ufuatiliaji wa siri wa Mchengerwa umebaini uwepo wa rushwa wazi wazi kuanzia kwa baadhi ya walinzi wasio waaminifu mpaka kwa watoa huduma na kauli mbaya zinazotolewa na walinzi hao na watoa huduma kwa wagonjwa.
Aidha wamekuwa wakiwafokea wagonjwa na kuwadhalilisha kinyume na maadili ya kazi yao.
Hivyo kufuatilia hali hiyo, Mchengerwa amemuelekeza Dk. Shekalaghe kufanya uchunguzi katika hospitali hiyo, kubaini chanzo cha changamoto hizo na hatimaye kuchukua hatua kwa mujibu wa kanuni na sheria za utumishi kwa wale watakaobainika kuhusika au kusababisha changamoto hizo.
Taarifa imeeleza kuwa mchengerwa ametoa wito kwa watumishi wote katika sekta ya afya nchini kubadilika na kwamba serikali haitasita kuchukua hatua watumishi wazembe, wala rushwa au wanaokiuka misingi ya maadili ya kazi zao.
Reviewed by Gude Media
on
December 26, 2025
Rating:

