Angalia mabondia walivyozichapa katika usiku wa Boxing Day

Bondia Hassan Mwakinyo, akitangazwa mshindi baada ya kumchapa bondia Stanley Eribo, kutoka nchini Nigeria, kwa Knock Out (KO), raundi ya pili, Warehouse, Masaki.




Bondia Debora Mwenda, akitangazwa mshindi baada ya kumtandika bondia Mariam Dick kutoka Malawi katika pambano la ubingwa wa mkanda PST. 




Mwamuzi akiwatangaza mabondia Leila Macho (kushoto) na Hidaya Zahoro, kuwa pambano lao ni droo.

Bondia Ally Mzome (kushoto), akisukuma konde kwa mpinzani wake Osana Arabi, ambapo Mzome aliibuka mshindi kwa points.

Bondia Hassan Ndonga (kushoto), akisukuma konde kwa mpinzani wake Ismail Boyka, ambapo Ndonga aliibuka mshindi kwa points


Mabondia Ramadhan Mkwakwate (kushoto) na Reagan Pacho, wakitafutana ulingoni katika pambano la kuwania mkanda wa PST, ambapo Mkwakwate aliibuka kuwa bingwa wa mkanda.

Bondia Ramadhan Mkwakwate, baada kutangazwa kuwa bingwa wa mkanda wa PST

Bondia Hamad Furahisha (kushoto), akipambana na bondia kutola Malawi, Hanock Phili, ambapo Furahisha, alishinda. 

Mshabiki wa ngumi wakishangilia mabondia wakizochapa ulingoni.

 

Angalia mabondia walivyozichapa katika usiku wa Boxing Day Angalia mabondia walivyozichapa katika usiku wa Boxing Day Reviewed by Gude Media on December 27, 2025 Rating: 5

Boxed Width - True/False

True