Saba mbaroni kwa tuhuma za wizi kwa njia ya mtandao - GUDE MEDIA

Breaking

GUDE MEDIA

Kila Sauti, Habari ni Yetu Sote

Subscribe Us

ads header

9/21/26

Saba mbaroni kwa tuhuma za wizi kwa njia ya mtandao


Na MWANDISHI WETU

Polisi kupitia Kitengo cha kuzuia makosa yanayohusu fedha (FCU), imewakamata watuhumiwa saba, akiwemo Steven Deogratius Mganga na raia wa China, Zhi Hang Wang kwa tuhuma za wizi kwa njia ya mtandao wa pesa zinazokadiriwa kuwa  shilingi bilioni mbili.

Taarifa kwa Umma, iliyotolewa na Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro, imeeleza kuwa matukio hayo yanadaiwa kutekelezwa katika mikoa ya Dar es Salaam, Dodoma na Tabora.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, mtuhumiwa Steven Deogratius Mganga ni miongoni mwa waliokamatwa, ambapo taratibu za kisheria zinaendelea.


No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.