Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), imeahidi kutimiza malengo ya Dira ya Maendeleo ya 2050, kwa kuanza ujenzi wa kujenga nyumba za gharama nafuu hususani kwa vijana.
Afisa Uhusiano na Mawasiliami wa TBA, Mtemi Sona amesema hayo kwenye Maonesho ya Kimataifa ya 50 ya Biashara maarufu SabaSaba yanayoendelea katika Barabara ya Kilwa, Dar es Salaam.
Amesema kupitia Dira ya Taifa yq Maendeleo ya 2050, TBA umeshaanza kutekeleza mipango huo wa kuwa na ujenzi wa mradi wa kujenga nyumba za makazi za gharama nafuu kwa kuanza ujenzi huo kwenye Wilaya ya Temeke Mkoa wa Dar es salaam na Jiji la Dodoma.
Aidha amesema nyumba hizo zitakuwa na chumba kimoja hadi viwili ambapo mwananchi wa hali ya chini ataweza kulipa gharama ndogo inayoanzia shilingi Laki 1 na kuendelea, ili kusudi aweze kuifadhi pesa itakayobaki kwa ajili ya kwenda kununua kiwanja cha kujenga nyumba yake mwenyewe.
Ameeleza lengo la TBA ni kwamba kila Mtanzania mwenye kipato kidogo hasa vijana wanaomaliza Vyuo Vikuu aweze kupanga nyumba hizo na baadae ana yeye aweze kuwa na makazi ya kumiliki nyumba yake mwenyewe.
Amesema kwa hivi sasa nyumba za gharama nafuu wameanza kuzijenga kwenye Wilaya ya Temeke Mkoa wa Dar es salaam na Mkoa wa Dodoma na baadae wataweza kwenda kujenga kwenye mikoa mingine iliyopo nchini.
Pia amewaomba wawekezaji wandani na wanje waweze kushirikiana na TBA katika kusaidia kifedha ili kujenga nyumba za gharama nafuu nchini, ili kila Mtanzania kupitia Dira ya Taifa ya Maendeleo ya 2050 aweze kumiliki nyumba hizo.


