Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, imesema inayozaidi ya shilingi Bilioni 22 kwa ajili ya kuwakopesha wajasiriamali mbalimbali.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Edward Mpogolo amesema hayo wakati alipotembelea kwenye banda la wajasiriamali wadogo na wakati wa Jiji la Dar es salaam kupitia maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa maarufu Saba Saba yanayoendelea kufanyika barabara ya Kilwa Jijini.
Katika ziara hiyo Mkuu huyo wa Wilaya ya Ilala aliambatana na Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam Nurdin Juma maarufu Shetta, Mkurugenzi Mtendaji wa Elihuruma Mabelya na Katibu Tawala wa Wilaya ya Ilala, Charangwa Seleman.
Mpogolo amesema wajasiriamali wa Mkoa wa Dar es Salaam wamekopeshwa fedha la fungu la asilimia 10 kwa ajili ya kuendeleza biashara zao na kujipatia kipato.
Amesema kupitia maonesho hayo wajasiriamali wameandaliwa dawati maalum kwa ajili ya kupatiwa elimu mbalimbali ikiwemo masuala ya kifedha.
Aidha Mpogolo ametumia nafasi hiyo kwa kumpongeza Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwa kuweza kutoa fedha za mikopo ambazo kwa hivi sasa zimeweza kuwanufaisha wajasiriamali hao.


