Shirika la Umeme Nchini (TANESCO), imewaletea wateja wao Huduma bora ya kisasa ya Nyumba janja ambayo husaidia kufanya marekebisho ya waya za umeme kwa kuepusha majanga ya mbaimbali yakiwemo ya moto yanayoweza kutoka kwenye nyumba zao.
Mkurugenzi wa Mawasiliano na Huduma kwa Wateja wa shirika hilo, Irene Gowele, amesema hayo katika Maonesho ya Kimataifa 50 ya Biashara (SabaSaba) yanayoendelea, Dar es Salaam.
Aidha amewataka wateja wao na watanzania kutembeea banda la TANESCO ili waweze kupata elimu na kujiunga na huduma ya teknolojia ya kisasa ya App kwa ajili ya usalama wa nyumba zao zisiweze kupata majanga ya moto.

