IGUNGA - TABORA
BALOZI wa Pamba nchini, ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mstafu, Aggrey Mwanri amewataka wakulima wa zao la pamba kuwa na badiliko la ghafla la tabia kuhusu kuendelea kuzalisha mbegu bora za zao hilo.
Balozi Mwanri ametoa wito huo, wakati wa semina kwa wakulima wa zao hilo wa kata za Mwamashiga, Itunduru na Mwamakona wilayani Igunga mkoani Tabora.
Aidha, amesema wanatoa elimu ya kuzalisha zao la Pamba safi ikiwemo mbegu yake kwa lengo la kuendelea kupata manufaa hasa kuzitumia fursa zitakazopatikana baada ya kujengewa kiwanda cha Kuchakata mbegu bora za zao hilo Wilayani Igunga.
Amedokeza kuwa katika zao la Pamba kuna utajiri wa kunukia kwa sababu katika zao hilo wanaweza kupata chakula cha mifugo, mafuta na malighafi za kutengenezea nguo.


