![]() |
| Mkurugenzi Idara ya Usimamizi, Uwajibikaji na Mahusiano JMAT, Leila Bhanji |
Na MWANDISHI WETU
Jumuia ya Maridhiano na Amani Tanzania (JMAT) imwataka wananchi, hususan vijana, kuacha kutumika vibaya katika mitandao ya kijamii kwa namna ambayo inaweza kuhatarisha usalama na utulivu wa nchi.
Wito huo umetolewa na Mkurugenzi Idara ya Usimamaizi, Uwajibikaji na Mahusiano kutoka JMAT, Leila Bhanji, katika Maonesho ya Kimataifa ya 50 ya Biashara, Barabara ya Kiwa, Dar es Salaam, huku ikisisitiza kuwa amani ya Tanzania ni tunu ya taifa inayopaswa kulindwa na kila mmoja.
Leila amesema taasisi hiyo inajumuisha Waislamu, Wakristo na waumini wa dini za kimila, huku msisitizo mkubwa ukiwa ni umoja bila ubaguzi wa aina yoyote.
"Sisi hatubagui dini, hatubagui kabila wala rangi, ikubwa ni kuwa na amani nchini Tanzania. Kazi yetu kubwa ni kuhakikisha tunaleta amani katika taifa letu na kuidumisha, pia kuweka maridhiano baina ya viongozi, wananchi wenyewe na serikali", amesema Leila.
Pia Leila amesema jumuia hiyo inasimamia umoja na mshikamano na kupiga vita utengano miongoni mwa jamii, kwani maendeleo ya nchi yanategemea utulivu, suluhu ya migogoro na huduma za jamii.
Pamoja na kuwakaribisha wenye changamoto au
migogoro mbalimbali kufika katika banda la JMAT lililopo Sabasaba au kwenye
ofisi zao ili kupata msaada wa kisheria na kijamii.



