Jinsi VETA Inavyowatengenezea Vijana Njia ya Kujiajiri Kupitia Ufugaji na Uzalishaji


Washiriki kutoka Mamlaka ya Mafunzo na Ufundi Stadi Tanzania (VETA) wamesema hawatamuangusha  Rais Dk. Samia Suluhu Hassan katika utoaji wa elimu bora kwa vijana wanaosoma kwenye Vyuo hivyo.

Kauli hiyo imetolewa na Mkufunzi mwandamizi kutoka Chuo cha VETA Mkoa wa Singida Dk. Jackson Mkopi alipokuwa akizungumza kwenye maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa maarufu Saba Saba wakiwa kama washiriki kwenye banda la VETA.

Amesema elimu wanayoitoa kwa vijana kupitia Chuo hicho ni pamoja na kujifunza ufugaji bora  wa wanyama, utengenezaji wa chakula cha mifugo na uzalishaji ambapo itawapelekea vijana kupata fedha na kuongezea pato la uchumi laTaifa.

Aidha Dk. Mkopi amesema VETA imeamua kufanya hivyo kwa ajili ya kuwataka vijana wanaomaliza elimu yao vyuoni kwa kupata ujuzi na maarifa, waweze kujitegemea kujiajiri na kuinua kipato chao.

Amefafanua kuwa katika kuelekea Dira ya Maendeleo 2050, Dk. Mkopi amesema Chuo hicho kinaendelea kutekeleza Dira hiyo kwa kubuni mambo mbalimbali yatakayowasaida vijana kuinuka kiuchumi.

Pia ametumia nafasi hiyo kwa kumpongeza Rais Dk. Samia kwa kila hatua anayopiga.anayopiga ya kuwaletea wananchi Maendeleo, hivyo na wao wamemuahidi hawatamuangusha katika utoaji wa elimu bora kwa vijana.

Hivyo ametumia nafasi hiyo pia, kwa kumpongeza Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mafunzo na Ufundi Stadi Tanzania (VETA) CPA Anthony Kasole kwa namna ya maandalizi bora aliyoyafanya katika maonesho ya mwaka huu, hasa kupitia banda la (VETA) kwani banda hilo limekuwa kivutio kwa watu wanaofika kutembelea maonesho hayo.