Kihongosi atembelea shina namba 7 Samaria tawi la Mnyoni, Singida



Na MWANDISHI WETU, SINGIDA

Katibu wa NEC Itikadi Uenezi na Mafunzo wa CCM), Kenani Kihongosi, ametembelea Shina Namba 7 la CCM katika Tawi la Manyoni Mjini, akiwa katika ziara kimkakati ya kuimarisha uhai wa Chama kuanzia ngazi ya mashina mkoani Singida.


Shina hilo lina wanachama 150, ambapo  Kihongosi amewashukuru wanachama na uongozi wa shina hilo kwa mshikamano, nidhamu na uongozi wao mzuri.


Kihongosi amesema kuwa, huo ndiyo utofauti wa CCM na vyama vingine, kwa kuzingatia muundo imara wa Chama, Katiba yake na uongozi madhubuti kuanzia ngazi ya taifa hadi mashinani.


Pia , Kihongosi amewasilisha salamu za Mwenyekiti wa CCM, Rais, Dk. Samia Suluhu Hassan, kueleza kuwa hata yeye ameendelea kujifunza misingi ya uongozi bora kutoka kwa viongozi wa mashina, akitaja Shina Namba 7 ni  mfano wa uongozi wa karibu na wananchi.



Kihongosi atembelea shina namba 7 Samaria tawi la Mnyoni, Singida Kihongosi atembelea shina namba 7 Samaria tawi la Mnyoni, Singida Reviewed by Gude Media on January 18, 2026 Rating: 5

Boxed Width - True/False

True