DAHRO Igunga Hamis awapongeza madereva wa serikali kwa kufanyakazi kwa weledi
MKUU wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu ( DAHRO) wa Halmashauri ya Wilaya ya Igunga mkoani Tabora, Hamisi Hamisi amewapongeza Madereva wa serikali kwa kufanya kazi zao kwa weledi na wakati.
Hamisi ametoa pongezi hizo wakati akiongea na Madereva hao katika kikao kazi kilichofanyika katika ofisi yake iliyopo katika Halmashauri hiyo mjini Igunga.
Amewahimiza kuendelea kutekeleza wajibu wao huku akiwaahidi kuzungumza na Wakuu wa Idara na Vitengo kwa lengo la kuhakikisha wanatoa stahiki za Madereva ambazo ni haki zao.
"Stahiki na haki ni lazima mpate kwa sababu ziko kisheria, hivyo endeleeni kutunza siri na kuwa waadilifu kazini," ameahidi.
DAHRO Igunga Hamis awapongeza madereva wa serikali kwa kufanyakazi kwa weledi
Reviewed by Gude Media
on
December 10, 2025
Rating:
Reviewed by Gude Media
on
December 10, 2025
Rating:



