JKCI kutoa matibabu bure kwa wananchi Mikoa ya Arusha, Moshi na Manyara
Na MWANDISHI WETU
TAASISI ya Moyo ya JaKaya Kikwete (JKCI), imewaka wananchi wa Mikoa ya Arusha, Manyara na Moshi kujitokeza kwa wingi kupata vipimo vya magonjwa ya Moyo na mengine yasiyo ambukizwa vitakavyofanyika bure katika Hospitali ya Lutheran Medical Center (ALMC), iliyoko jijini humo kuanzia Desemba 29 hadi Januari 5 mwakani.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI, Dk.Piter Kisenge, amesema hatua hiyo inatokana na dhamira ya dhati ya serikal inayoongozwa na Rais Dk.Samia Suluhu Hassan ya kuokoa maisha ya wananchi na kuboresha huduma za afya.
"Wananchi wa Arusha na Mikoa jirani wajitokeze kwa wingi kupata matibabu hayo bure, hatua hii ni mwendelezo wa kampeni yetu ya Dk.Samia Tiba Mkoba ya kuwafikisha wananchi huduma za afya ya Moyo karibu.Pia Tunamshukuru Rais Dk.Samia kwa kutoa fedha za kufanikisha matibabu bure ya Moyo kwa wengi,"amesema.
Amesema dhamira ya JKCI kuendelea kutoa huduma hizo ni kuhakikisha wananchi wanapata huduma za matibabu ya Moyo na hakuna anayepoteza maisha kwa kukosa huduma hizo.
Kwa upande wake, Maneja wa kitengo Cha Mawasiliano Cha Bohari ya Dawa Nchini (MSD), Etty Kusiluka aliipongeza JKCI kwa hatua hiyo kubwa huku akiahidi ushirikiano kufanikisha kambi hiyo.
Reviewed by Gude Media
on
December 22, 2025
Rating:
