Mbeto ampasha OMO Wazanzibari wamechoshwa na maisha ya hasama
Na Mwandishi wetu , Zanzibar
Cha Mapinduzi kimemtaka Mwenyekiti wa ACT Wazalendo Othman Masoud Othman kuacha porojo na kuwapotosha wananchi kwa kupandikiza maneno ya hasama na chuki katika jamii huku akiahidi mambo yasiowezekana.
Vile vile, CCM kimesisitiza kuwa Uchaguzu Mkuu umeshamalizika, wananchi wametumia haki yao ya kikatiba na kidemokrasia kwa kuiweka Serikali walioitaka madarakani.
Matamshi hayo yametamkwa na Katibu wa Kamati Maalum ya NEC Zanzibar, Idara ya itikadi, Uenezi na Mafunzo, Khamisi Mbeto Khamis aliyemtaka Othman kukubali ukweli ameshindwa Uchaguzi kutokana na nguvu ya maamuzi ya wengi.
Mbeto alisema Othman hana sababu zenye mashiko ,bali anajaribu kuidanganya dunia akidai yeye ndiye mshindi wakati Tume ya Uchaguzi Zanziabr imeshamtangaza mgombea aliyeshinda Urais .
Alisema Othman asingeweza kumshimda mgombea wa CCM Rais Dk Hussein Ali Mwinyi kwa sababu kadhaa muhimu ambazo zina ukweli usiokwepeka.
'Othman alikuwa akiomba nafasi y kuchaguliwa ili awatumikie wananchi wa Zanziabr. Rais Dk Mwinyi alishapimwa jinsi ilivyoitumikia nchi na watu miaka mitano iliopita. Ndoto ya OMO ni kuleta Maendeleo wakati mwenzake alishafanya kazi ya kuleta maendeleo inayoonekana" Alisema Mbeto
Aidha, Katibu huyo Mwenezi alisema fikra na hesabu za Othman ? alidhani wananchi wangembagua na kumchukia Rais Dk Mwinyi kutokana na matamshi ya Makamu wake Mwenyekiti Ismail Jussa Ladhu alivyokuwa akitumia hutuba za ubaguzi kama sera na mtaji wa kupata ushindi.
"Zanzibar nchi ya Visiwa. Ni mkusanyiko na mkutanisho wa watu toka pembe nyingi za dunia .Unapoonyesha au chama chako kina sera za kibaguzi unalazimisha upigiwe kura za chuki dhidi yako" Alieleza
Pia Mwenezi huyo alisema miaka mitano iliopita utawala wa Rais Dk Mwinyi, umewaunganisha wananchi waliogawanyika kwa siasa za chuki .Ameongoza bila kujali asili zao ,rangi walizonazo ,Siasa au itikadi za vyama vyao.
"Ka miakaa mitano iliopita Wazanzibari waliishi kwa utulivu kama maji ndani ya mtungi. Wamekuwa wamoja ,wenye upendo mshikamano. Hazikusikika sauti za kubaguana, kusimangana wala kuhitilafiana "Alisisitiza
Mbeto alimtaja kiongozi pekee ambaye kila wakati alisikika katika mkutano yake akijaribu kuwagawa wananchi asili,nasaba na siasa ili kuwavuruga kwa historia na matukio ya kisiasa yaliopita ni Jussa peke yake.
"Kushindwa kwake OMO kwa sehemu kubwa kumeporomoshwa na aina ya utata wa Siasa na matamshi ya Jussa. Wazanzibari wamwchoshwa na heka heka za kubaguana na kugombanishwa kwa itikadi za vyama"Alisema Mwenezi huyo.
Reviewed by Gude Media
on
December 20, 2025
Rating:
