Halmashauri ya Igunga imejipanga kuhakikisha wanafunzi wote wanaendelea kufaulu kwa asilimia zote
IGUNGA - TABORA
KUELEKEA muhula mpya wa elimu 2026, viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Igunga mkoani Tabora wamejipanga vema kuhakikisha Wanafunzi ngazi ya Awali, Msingi na Sekondari wanaendelea kufaulu kwa asilimia 100.
Akizungumza na Watumishi wa Masijala, Maofisa Waendesha Ofisi na Idara za Elimu Msingi na Sekondari wanaofanya kazi Makao Makuu ya Halmashauri hiyo, Mkuu wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu ( DAHRO), Hamisi Hamisi amewakumbusha Wakuu wa Idara hizo kuendelea kuwajali Walimu.
Aidha, amewaomba viongozi hao kuendelea kutoa taarifa kwa Mwajiri kwa wakati ikiwa kunawalimu ni watoro kazini na kuwafahamu watumishi wanaotarajia kustaafu kwa lengo la kuandaa stahiki zao mapema.
Pia, amewakumbusha kutenga bajeti ambayo itatumika kutoa mafunzo ya awali kwa walimu ambao wanaajiriwa kwa sababu itawasaidia kuepuka malalamiko, lugha zisizo na staha na kushitaki kwa mwajiri wao mara kwa mara.
Reviewed by Gude Media
on
December 11, 2025
Rating:


