Balozi Mulamula amlilia Jenista Mhagama
Na MWANDISHI WETU
Mjumbe Maalum wa Umoja wa Africa kuhusu Wanawake Amani na Usalama, Balozi Liberata Mulamula, amesema amepokea kwa masikitiko makubwa na mshtuko taarifa za kifo cha Mhe. Jenista Mhagama huku akisema ni pigo kubwa sana kwa nchi yetu na jamii ya Watanzania kwa ujumla.
Akizungumza na Mwandishi wetu leo, amesema Taifa limepoteza mwanamke jasiri na hodari wa kazi aliyehudumu kwa weledi mkubwa katika nafasi mbalimbali muhimu Serikalini.
"Namkumbuka sana alivyonipokea Bungeni kwa mara ya kwanza kwa unyenyekevu mkubwa akiwa 'Chief Whip’ baada ya mimi kuteuliwa na Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kuwa Mbunge na Waziri wa Mambo ya Nje mnamo mwezi Machi 2021," amesema.
Ameeleza kuwa, kiongozi huyo alikuwa mwepesi wa kuelekeza, kiongozi shupavu na mnyenyekevu. Nilijifunza mengi kutoka kwake kuhusu kuchangia hoja Bungeni na kwa umakini.
"Namkumbuka kwa ucheshi wake na tabasamu lake wakati wote. Alikuwa mcha Mungu sana na tulisali wote Parokia moja ya Kiwanja cha Ndege Dodoma. Hakika tumempoteza Kiongozi makini, mchapa kazi na mpenda watu. Tutamkumbuka daima.
Bwana ametoa Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe. Amina,"
Reviewed by Gude Media
on
December 12, 2025
Rating:
