Askofu Kikoba wa Kanisa la Injili Hasa ya Yesu Kristo ameasa Taifa kuendelea kuenzi amani, upendo na umoja


Na MWANDISHI WETU

ASKOFU  wa Kanisa la Injili Hasa  ya Yesu Kristo (Actual Gospel Of Jesus Christ Church), Mataro Kikoba amewaasa Watanzania kushirikiana kwa pamoja kulirejesha taifa la Tanzania katika misingi yake ya awali ya upendo, umoja na amani.

Akizungumza waandishi wa habari Jijini Dar es salaam  waliofika kanisa hapo kushuhudia tendo la ndoa takatifu Askofu kikoba   ambapo pia alitumia mahubiri yake kutoa Ushauri kwa watanzania .

Askofu Kikoba amesema nivema kukumbuka misingi  ambayokwa namna moja ama nyingine ilitikiswa hasa kutokana na vurugu zilizojitokeza Oktoba 29, mwaka huu.

Amesema Watanzania hawana sababu ya kugawanyika kwa namna yoyote ile akidai kuwa taifa linapaswa kuwa moja na la mfano kote duniani.

“Taifa pamoja na kuwa na watu wenye mitazamo tofauti tofauti halipaswi kugawanyika na kupoteza malengo yake, linatakiwa kuwa imara na kuendesha shughuli zake mithili ya wizara ya elimu.

“Wizara ya Elimu, namna wanaendesha sekta ya elimu katika mazingira tofauti tofauti unaweza kufikiri labda watapoteza dira lakini walimu wanafundisha kitu kinachofanana kwa wanafunzi wote,” amesema huku akidai kuwa kama ilivyo kwenye elimu neno la Mungu nalo linapaswa kuwarejesha Watanzania kuwa pamoja na wamoja.

Kiongozi huyo wa kanisa lililoanzishwa mwaka 2002 na makao yake makuu yakiwa hapa Tanzania ,Mtoni Mtongani,Mtaa wa Kichangani anapongeza Watanzania na serikali kwa ujumla kwa kuimarisha amani na kuwaasa katika kipindi hiki cha kuelekea mwishoni mwa mwaka 2025 kwenda mwaka mpya 2026, wazidi kumuomba Mungu amani na usalamaa vizidi kutawala.

“Neno la Mungu kwenye biblia hasa kitabu cha Luka sura ya 10 mstari wa 27, Mungu ameweka amri 10 lakini kuna mahali ameziunganisha katika amri kuu mbili tu; upendo uweze kutawala na watu tuwapende jirani zetu.

“ Ndugu zangu tukifanya hivyo tayari tunakuwa tumejenga kitu kimoja kikubwa sana ambacho ni amani, na hii ndio tunu ya taifa ya msingi mno kuliko tunu nyingine zote kwenye taifa,” amesema.

Pamoja na msingi wa amani ya taifa kutikiswa baada ya kuwa imara kwa kipindi kirefu amesema ni wazi kuwa Watanzania sasa wamepata kutambua kuwa amani ndio msingi kwenye maisha ya kila mtu hivyo ni muhimu wakazidi kuiimarisha ili izidi kutawala kuanzia mtu mmoja mmoja na jamii yote kwa ujumla.

Ametoa ushauri kwa viongozi kutawala kwa mapenzi ya Mungu akieleza wazi kuwa hata kwenye vitabu vya dini imeelezwa kuwa uongozi wowote hapa duniani umetoka kwa Mungu hivyo kwa kuamini hilo viongozi wote wanapaswa kutawala kwa matakwa ya Mungu.

Sambamba na hilo amesema agizo la Mungu kwa wanadamu ni kuzaana na kuongezeka duniani ambapo pamoja na agizo hilo aliwataka kuwa na wajibu huku ajitaja wajibu mmojawapo kuwa ni binadamu kuwa watiifu.

“Katika kitabu cha Waefeso sura ya tano mstari wa 22 Mungu ametoa wajibu kwa kila mmoja wetu.

Alianza na mwanamke kwa kumuelekeza kuwa awe mtiifu kwa mme wake, leo duniani ndoa zimekuwa na changamoto nyingi kwa sababu wanawake walio wengi wamekosa kujua wajibu wao, wamekosa utii kwa waume zao.

“Vurugu na mifarakano siku hizi inaanza ndani ya ndoa takatifu, kwa vile mwanamke aliamriwa kuwa mtiifu kwa mme wake, mwanaume naye amepewa agizo la kupenda, sasa unaweza kuona kuwa wanaume nao hawawezi kutimiza agizo la kupenda wake zao ikiwa hawana utii kwao,” amesema.

Na kuongeza kuwa jamii nzima hasa wanaume na wanawake kutekeleza wajibu waliopewa na Mungu wa upendo na utii akidai kuwa wajibu huo ukitimizwa utaepusha ongezeko la wajane na yatima kwenye jamii.

Kwa upande mwingine ametoa wito kwa vijana akiwaomba nao kutimiza wajibu wao kwa kuhakikisha wanajishughulisha katika kazi mbalimbali za kuwaletea maendeleo.

Anaeleza kuwa endapo vijana watahakikisha kufanya kazi kwa bidii ni wazi kuwa jamii yote kwa ujumla pamoja nataifa zima litarejea kwenye sifa yake ya awali ya kuwa kisiwa cha amani na litastawi na kustawisha Watanzania wote.

Askofu Kikoba wa Kanisa la Injili Hasa ya Yesu Kristo ameasa Taifa kuendelea kuenzi amani, upendo na umoja Askofu Kikoba wa Kanisa la Injili Hasa ya Yesu Kristo ameasa Taifa kuendelea kuenzi amani, upendo na umoja Reviewed by Gude Media on December 30, 2025 Rating: 5

Boxed Width - True/False

True