Wananchi Igunga wahimizwa kutunza mazingira - GUDE MEDIA

Breaking

GUDE MEDIA

Kila Sauti, Habari ni Yetu Sote

Subscribe Us

ads header

8/18/24

Wananchi Igunga wahimizwa kutunza mazingira

IGUNGA - TABORA

MKURUGENZI Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Igunga mkoani Tabora, Selwa Abdalla Hamid akishirikiana na mmoja wa wakimbiza Mwenge wa uhuru kitaifa 2024, Makwaya Joseph kupanda miti kwa lengo la kuendelea kutunza mazingira.

Viongozi hao, wamepanda miti hiyo leo katika shule ya Sekondari Mwakipanga katika wilaya hiyo  mkoani hapa wakati wa mbio za Mwenge wa Uhuru ulipotembelea eneo hilo.

Akitoa salamu za mbio za Mwenge wa Uhuru katika eneo hilo mmoja wa wakimbiza Mwenge kitaifa,  Makame Ramadhani Hamis aliwahimiza wananchi kuendelea  kutunza mazingira kwa lengo la kuendelea kukuza uchumi wao na wa Taifa.

"Ndugu zangu wananchi ukikata mti unatakiwa upande mti," amesisitiza.




No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.