Mkurugenzi Aagiza Wananchi Wanaoishi Mabondeni Kuhama Mara Moja


IGUNGA - TABORA

MKURUGENZI Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Igunga mkoani Tabora, Selwa Hamid amewataka Watendaji wa Kata na Vijiji kutoa matangazo ikiwemo kutumia radio jamii kuwaeleza wananchi wanaoishi sehemu za mabonde wahame kwa sababu inadaiwa mvua zitakuwa kubwa zinazoweza kuleta mafuriko.

DED Selwa ametoa agizo hilo, wakati alipokutana na Watendaji hao katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri hiyo mjini Igunga.

Aidha, amewaagiza Watendaji hao kuwaeleza Wafanyabishara na Wananchi ambao mbele yao kuna mitaro waisafishe kwa lengo la kuhakikisha maji yanayodaiwa kuwa machafu yasikwame katika maeneo hayo.

"Kila mmoja afanye oparesheni katika maeneo yake kusafisha mitaro kabla ya mvua kuanza kwa sababu baada ya mvua kuanza hawataweza kufanya hivyo," amesisitiza.