DC Mpogolo Awataka Watendaji Kufanyakazi kwa Weledi na Kukemea Rushwa


Na MWANDISHI WETU

MKUU wa Wilaya ya Ilala Edward Mpogolo, amewataka Watendaji wa Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam kufanya kazi kwa weledi na kusimamia miradi  ya Serikali  iweze kukamilika kwa wakati huku akiwaonya  katika usimamizi wa miradi hiyo kukemea vitendo vya rushwa.

Mpogolo ,alitoa agizo hilo kata ya Chanika na Zingiziwa wilayani Ilala katika  kampeni ya kupanda miti na usafi wa Mazingira.

"Natoa onyo Viongozi na Watendaji dhidi ya vitendo vya rushwa na matumizi mabaya ya fedha za Serikali na kujadili maslahi binafsi yanayoweza kuhusishwa na mikataba au miradi inayotekelezwa na Serikali katika masuala ya rushwa"amesema Mpogolo. 

Mpogolo amesema, kazi ndio kipimo kikubwa cha uongozi hivyo wanapaswa kukaa na kujadili namna ya kufanya kazi vizuri, na kuhakikisha miradi inakamilika kwa wakati na namna wananchi wanavyopata huduma bora sio vizuri Viongozi au Watendaji kukaa na kujadili ni asilimia gani ya fedha wanapata kutokakana na mikataba au miradi ya Serikali  

Aidha amesema fedha zinazotengwa na Serikali kwa ajili ya ujenzi wa Barabara au miundombinu ya sekta ya afya au sekta ya Elimu na huduma zingine za umma hivyo kila kiongozi au Mtendaji ana wajibu wa kuhakikisha zitatumika kwa uadilifu ,uwazi,kwa kuzingatia thamani ya fedha (value for maney)ili wananchi waweze kupata manufaa yaliokusudiwa.

Amesema Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam na Wilaya ya Ilala imeona nidhamu na uadilifu katika usimamizi wa fedha alitumia fursa hiyo kuwapongeza sana Viongozi wa Halmashauri hiyo na kuwataka wasibweteke waendelee kuchapa kazi na kuwa wadilifu kwa sababu uadilifu ndio msingi wa Serikali yenye kuwajibika.

Kwa upande mwingine alitumia fursa hiyo kuwataka Viongozi kujenga Utamaduni wa kufanya kazi kwa kushirikiana ,kusimamia miradi ya maendeleo ya Serikali na kuhakikisha kila rasilimali inayotolewa  na Serikali inalenga kuboresha maisha ya wananchi na si kutengeza maslahi binasfi

Aliwataka Watendaji wa  Serikali, kuanzia ngazi ya Serikali ya mtaa hadi wilaya kuwa karibu na Wananchi kusikiliza na kushughulikia changamoto zao kwa wakati huku akisisitiza kuwa Viongozi hao wameaminiwa na Serikali ili wawe sehemu ya suluhisho la kutatua kero zao.

"Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan ,amekuwa akihakikisha Serikali inapata fedha kwa ajili ya utekelezaji wa mradi ya maendeleo katika maeneo mbalimbali nchini,hivyo ni wajibu wa Viongozi waliopo katika maeneo hayo kuhakikisha miradi hiyo inatekelezwa kwa ufanisi na kuwanufaisha wananchi, "amesema.