IGUNGA - TABORA
KATIBU Tawala wa Mkoa wa Tabora, Dk. John Mboya amempongeza Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa anayoendelea kuifanya kwa lengo la kuhakikisha nchi inaendelea kupata maendeleo.
Dk. Mboya ametoa pongezi hizo katika Baraza la Madiwani, kupokea taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ya hesabu za Halmashauri ya Wilaya ya Igunga ambayo imepata Hati Safi.
Pia, amewapongeza viongozi wa halmashauri hiyo kwa kusimamia miradi ya maendeleo, ambayo serikali imeendelea kuleta fedha nyingi katika sekta ya afya, elimu, barabara, umeme, maji na utawala.
"Katika ukaguzi wa hesabu wa Serikali za mamlaka za mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Igunga imepata Hati Safi na Halmashauri nyingine zote za mkoa wetu zimepata Hati Safi, Hongereni sana," amepongeza Dk. Mboya.



