Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri Igunga Apongeza Kikosi Kazi Kukusanya Mapato


IGUNGA - TABORA 

MKURUGENZI Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Igunga mkoani Tabora, Selwa Hamid amewapongeza Watumishi waliyopo katika kikosi kazi cha kukusanya mapato kwa kazi nzuri ambayo wanaendelea nayo.

Selwa ametoa pongezi hizo, wakati akigawa pikipiki kwa watumishi waliyoko katika kikosi kazi hicho katika viwanja vya Halmashauri hiyo mjini Igunga.

Amesema mapato ya ndani yamewezesha kununuliwa pikipiki ambazo zimegawiwa kwa baadhi ya watumishi waliyopo katika kikosi kazi hicho ambapo wanaamini zitapunguza adha wakati wanafuatilia mapato katika maeneo tofauti.

"Ni jambo la busara kuwapatia pikipiki hizi kutoka kwenye mapato yetu ya ndani ziwasaidie kupunguza nguvu kubwa mnazozitumia katika kukusanya mapato," amesema.