DAHRO Igunga awataka watumishi kuendelea wajibu wa kufanya kazi kwa bidii na weledi
IGUNGA - TABORA
MKUU wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu ( DAHRO) wa Halmashauri ya Wilaya ya Igunga mkoani Tabora, Hamisi Hamisi amewasihi watumishi kuendelea kutekeleza wajibu wa kufanya kazi kwa bidii kwa sababu serikali inaendelea kupandisha vyeo watumishi wa umma wenye vigezo.
Hamisi ametoa wito huo wakati akiongea na Watumishi wa Idara ya Afya katika Ukumbi wa Hospitali ya Wilaya mjini Igunga.
Akiongelea kuhusu makosa ya kinidhamu, Hamisi amewashauri kutokua na tabia ya wizi na rushwa ikiwemo wizi wa dawa ambazo zimeletwa na serikali au kuchukua dawa kwa kutumia kadi za watu wengine.
Aidha, amewasisitiza kuziishi kanuni za maadili ya utendaji katika utumishi wa Umma ikiwemo kutoa huduma bora, kutoa huduma bila upendeleo, kufanya kazi kwa uadilifu, kuwajibika kwa umma, kuheshimu sheria na kuwa na Matumishi sahihi ya taarifa.
Reviewed by Gude Media
on
December 12, 2025
Rating:

