DC Kahama ajivunia matunda ya kodi wilayani kwake

 


Na MWANDISHI WETU

Mkuu wa Wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga, Mboni Mhita,  amewataka wananchi kuendelea kulipa kodi na kujivunia maendeleo  yanayopatikana kutokana na kodi wanazolipa. 

Mboni ameyasema hayo leo Machi 18, 2025  alipokutana na maofisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), waliofika ofisini kwake  kujitambulisha katika  kampeni ya elimu ya kodi ya mlango kwa mlango inayoendelea wilayani humo.

Amesema ndani ya Wilaya kuna miradi ambayo inatokana na kodi wanazolipa wananchi.

"Kodi tunalipa ndiyo  zinatumika na serikali kufanya maandaleo haya katika jamii, sisi wa Kahama tunajivunia hospitali ya kisasa inayofanana na kanda, ukiangalia zahanati za kisasa katika wilaya yetu", amesema.

Kwa upande wake, Ofisa Mkuu Msimamizi wa kodi TRA, Lameck Ndinda,  amesema  lengo la kampeni hiyo ni kutoa elimu ya kodi na kusikiliza changamoto na maoni ya wafanyabiashara ili kuweza kuboresha huduma zao 

Ndinda amesema wamebaini kuna baadhi ya wafanyabiashara bado hawajakadiriwa na na wengine kutokutoa risiti vizuri.

Aidha, Ndiba ametoa wito kwa wafanyabiashara kwenda kukadiriwa kabla ya tarehe 31 Machi ili kuepuka adhabu.

"Wito wangu kwa wafanyabiashara kujitokeza kwa wingi kwenda kukadiriwa kabla ya tarehe 31 mwezi Machi, na wakisha kukadiriwa wawahi kufanya malipo ya awamu ya kwanza", amesema.

Naye, mmoja wa wafanyabiashara,  Tumaini Kinanda,  amesema kampeni hiyo inasaidia kuboresha uhusiano kati ya TRA na wafanyabiashara.

Kinanda ameomba kampeni hiyo iwe endelevu waweze kujifunza zaidi mambo mbambali ya kodi.






DC Kahama ajivunia matunda ya kodi wilayani kwake DC Kahama ajivunia matunda ya kodi wilayani kwake Reviewed by Gude Media on 9:32:00 AM Rating: 5

No comments

Note: Only a member of this blog may post a comment.