Twanga Pepeta ya peleka burudani New Wallet Pugu


Na MWANDISHI WETU

BENDI ya muziki wa dansi ya The Arican Stars  Internatiobal ‘Twanga Pepeta’  inatarajia kufanya onesho kubwa na la aina yake katika Ukumbi wa New Wallet  Pub, uliopo Kwa Rais, Kata ya Pugu, Ilala, jijini Dar es Salaam.

 Onesho hilo linatarajiwa kufanyika  Julai 19 mwaka huu  na litakuwa halina kiingilio.

Akizungumza na  waandishi wa habari, jijini Dar es Salaam, Mwandaaji wa onesho  hilo, Emmanuel Tengia, amesema, onesho hilo la Twanga Pepeta ni mwanzo tu wa mfurulizo wa burudani katika ukumbi huo na Kata ya Pugu.

“Tulianza na bendi ya Msondo, awamu hii tunashusha kikosi kizima cha Twanga Pepeta. Onesho litakuwa kubwa na tumejipanga vyema kuhakikisha mashabiki watakao ingia ukumbini wanakata kiu,”amesema Tengia.

Ameeleza,  hakuta kuwa na kiingilia kwa mashabiki  na watatakiwa kununua kinywaji au chochote ukumbini.

Tengia, ameeleza  dhamira ni  kuhakikisha  wananchi wa Kata ya Pugu na viunga vyake wanapata  eneo la burudani na starehe.

"Kata ya Pugu hakukuwa na eneo  maalumu ambalo wananchi wanaweza kupata burudani za bendi kubwa hapa nchini. New Wallet tumeamua kuwasogezea burudani hiyo. Baada ya Twanga Pepeta bendi itakayofuata ni FM Academia."ameeleza.



Twanga Pepeta ya peleka burudani New Wallet Pugu  Twanga Pepeta ya peleka burudani  New Wallet Pugu Reviewed by Gude Media on 4:17:00 AM Rating: 5

No comments

Note: Only a member of this blog may post a comment.