Mbeto amvaa Zitto akimtaka aache Ubaguzi na kudhalilisha utu wa watu.

Mwandishi  Wetu, Zanzibar

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimelaani matamashi ya Kiongozi Mstaafu wa ACT Wazalendo  ,Zitto Kabwe, aliyeshangazwa na kujitokeza waandishi  wa habari, watangazaji, waigizaji na wachekeshaji waliochukua fomu  za kuwania  Ubunge. 

Vile vile, CCM kimemtaka Zitto ambaye ni Mbunge wa zamani wa Kigoma Mjini, kutambua hata wenye  taaluma hizo, nao ni binadamu kama wengine. 

Akizumgumza katika Ofisi Kuu ya CCM  Kisiwandui  Kisiwani Unguja, Katibu  wa Kamati  Maalum  ya NEC Zanzibar, Idara ya Itikadi na Mafunzo, Khamis  Mbeto  Khamis, ameyaita matamshi hayo ya Zitto  ni ubaguzi  wa wazi.

Mbeto amesema demokrasia ya Uchaguzi haibagui watu kwa rangi zao, Kabila, Dini au kwa kada zao Kitaaluma , badala yake kila mtu  ana haki na  Uhuru wa kuchagua au kuchaguliwa.

Amesema  wakati  Zitto akiwaponda   Waandishi  wa Habari, Watangazaji,  Waigizaji  na Wachekeshaji, Taifa la Ukraine  hivi sasa, linaongozwa na Rais wake ambaye ni Mchekeshaji Volodymyr  Zelensky.

Zelensky amezaliwa Januari 25 Mwaka 1978  ni Mwanasiasa, Mwandishi na Mwigizaji wa filamu, Mchekeshaji na sasa ndiye Rais wa  Ukraine. 

"Zitto  ametoa matamshi ya dharau, kebehi na dhihaka iliopitiliza dhidi ya  taaaluma hizo duniani  kote . Alichokifanya ni unyanyasaji na udhalilishaji mbele ya macho ya dunia", amesema Mbeto.

Aidha, Mbeto amesema CCM  kina wanachama wenye  taaluma na fani mbalimbali, hivyo  hakitawazuia watu fulani ili kuwaruhusu kundi fulani, wachuke fomu na wengine  wazuiwe. 

"CCM  ni taasisi  kubwa ya kisiasa yenye  wanachama toka makundi  ya watu wenye uelewa, ufahamu,fani na taaluma kadha wa kadha.  Istoshe si chama cha kibaguzi aidha kwa dini, rangi au asili za watu " Alieleza 

Amesema imekuwa ada na kawaida ya viongozi wa  ACT  Wazalendo , mara  kadhaa kutumia   lugha  za kubagua watu kwa asili zao , nasaba na kabila ,huku wakikdhani hiyo ndio siasa safi. 

"Hakuna makundi ya watu wenye alama na kusema  hawa wanafaa kwa urais, ubunge  ,udiwani au uwakilishi  na wengine wasifae . Katiba ya nchi inataja usawa kwa binadami wote mbele ya katiba na sheria", amefafanua  Mbeto.

Mbeto amemtaka zitto kutoka na kusimama hadharani ili kuwaomba radhi waandishi  wa habari ,waigizaji na wachekeshaji kutokana na matamshi  yake yalioonyesha dharau ,Ubaguzi na udhalilishaji.

Mbeto amvaa Zitto akimtaka aache Ubaguzi na kudhalilisha utu wa watu. Mbeto  amvaa Zitto akimtaka aache Ubaguzi na kudhalilisha utu wa watu. Reviewed by Gude Media on 1:50:00 AM Rating: 5

No comments

Note: Only a member of this blog may post a comment.