Halmashauri ya Wilaya Igunga yampongeza Rais Dk. Samia kuimarisha Hifadhi za Taifa

Na MWANDISHI WETU, SERENGETI

MKUU wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu wa Halmashauri ya Wilaya ya Igunga mkoani Tabora, Hamisi Hamisi ameishukuru serikali inayoongozwa na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwa namna  ilivyoimarisha Hifadhi za Taifa jambo ambalo linawavutia watalii wengi.

Hamisi ameyasema hayo wakati alipowaongoza watumishi wa halmashauri hiyo, kufanya ziara ya kutembelea Hifadhi ya Taifa ya Serengeti wilayani Serengeti mkoani Mara.

Amesema serikali ya Rais Dk. Samia imeimarisha vivutio vya utalii hususan Mbuga ya Serengeti ambapo  miundombinu imeboreshwa kwa kasi kubwa, hivyo kuvutia watalii kwa wingi kutoka ndani na nje ya nchi.

Naye Mtendaji wa Kata ya Isakamaliwa,  wilayani Igunga, Misambo Kanyelele amesema wamefanikiwa kuona Nyumbu, Simba, Twiga, Viboko, Swala paa, Pundamilia, tembo, kobe, nyamera, swala Tom, chui, viboko, Mamba  wakiwemo ndege aina ya Mbuni, Kanga na Kware.